Home / Web Design / Tupakue na Kufanya Configurations na Installition ya WordPress

Tupakue na Kufanya Configurations na Installition ya WordPress

1Habari.

Asante kutembelea website ya yesayasoftware.com, leo nitakuonyesha jinsi ya kupakua WordPress. Tembelea website ya WordPress wordpress.org, utaona link ya kupakua WordPress, utaenda kwenye link ya kupakua WordPress, wakati narekodi video hii WordPress iko toleo namba 4.4.1.

Ukimaliza pakua WordPress, nenda kwenye Folder la Downloads kisha unzip file ulilodownload. Unaweza angalia mafile yalio ndani ya folder la wordpress, lakini muhimu hapa inatakiwa uhamishe folder la wordpress kwenda kwenye WAMP ndani ya folder la www.

Hatua inayofuata ni kutengeneza database, mimi nimetumia navicat, unaweza tumia chagua lingine kama phpmyadmin na kutengeneza database. Nimeiita website kama jina la database ambako WordPress itatunza taarifa kuhusu website, kisha rudi kwenye browser na fungua link ya localhost/wordpress ili uanze fanya configurations na installation ya WordPress.

Kuna hatua mbalimbali wakati wa kufanya configurations and Installation ya WordPress, link ikifunguka chagua lugha, na hapa chagua ni lugha ya kiingereza. Utapata maelezo ya taarifa unazopaswa jua kuhusu database kisha bonyeza Let’s go. Baada ya hapo andika jina la database uliotengeneza, mimi niliandika website, kisha ingiza username, password na host na hapo acha hiyo localhost, pia acha table prefix hiyo hiyo unaweza badili pia mimi nilibadili kuwa yes. Ukimaliza bonyeza Submit, kisha Run the Install.

Ikimaliza andika jina la website, kwenye video hii nimeandika Mafunzo, User andika jina lako mimi nimeandika langu, kisha weka password utayotumia ingilia kwenye WordPress. Unaweza weka na email yako pia kisha Install WordPress.

Nafurahi tumefika kwa pamoja hatua hii, tumeweza pakua na kufanya Configurations na Installation ya WordPress. Usiende mbali na yesayasoftware.com, ungana nami kipindi kijacho tukiingia ndani zaidi kwenye WordPress.

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Beginners or those who have taken a break from web design for a few years …

  • Neema Rajabu

    Great! WordPress is super easy.

  • Neema Rajabu

    Woww..Wordpress is awesome,! seems to be easy and superfast in creating websites