Home / Graphic Design / Tengeneza Infographics na Adobe Illustrator Hatua Nilizopitia

Tengeneza Infographics na Adobe Illustrator Hatua Nilizopitia

Kuna wakati ungependa elezea taarifa flani kwa njia ya graphs au charts na wengi tumekuwa tukitumia spreadsheets kama excel kwa muda sasa. Infographics inapeleka mbele zaidi wazo hili kwa kutengeneza story juu ya taarifa unayotoa.  Juzi nilikuarifu juu ya Infographics, tayari nimemaliza project hii na hapa nitashare hatua nilizopitia.

Katika project hii nilijiuliza maswali kadhaa, kwanza taarifa ipi nataka ifanyia kazi? Na wapi nitapata report ya kuniongoza kukamilisha jambo nalo taka fanya. Mimi ni mdau wa Teknohama niliona itakuwa vyema wazo langu likijikita huko. Pili nilipenda tumia taarifa za hapa Tanzania.

Uzuri, ninafahamu mamlaka ya mawasiliano (TCRA) hutoa ripoti juu ya mwenendo wa mawasiliano kila baada ya miezi mitatu. Hivyo, nilitembelea website ya TCRA na kuangalia ripoti juu ya taarifa za mawasiliano iliyotoka mwezi machi. Nilipata muda pitia ripoti hii, na nilichagua vipengele viwili ambavyo niliona vitatengeza stori kwenye design yangu. Nilichagua taarifa katika kipengele namba 1.1 (a) pamoja na 2.4.

Baada kujibu maswali yangu na kupata taarifa kuhusu maswali niliojiuliza nilifungua Adobe Illustrator, mimi ninatumia Adobe Illustrator CC toleo ya 2015 pamoja na update zake za mwezi November ambayo imepewa namba za toleo 19.2.1.

Hapa kwenye Adobe Illustrator tool niliotumia kwa kutengeneza graphs ni Graph Tool. Sikupata shida kuhusu rangi, nilitumia rangi za kampuni husika. Pia sikuwa na haja redesign logo za haya makampuni ili kupata vector image, nilitumia image trace feature ya Adobe Illustator na kupata vector image.

Cha msingi hapa hakikisha design yako inaleta stori Fulani , na pia kuna muendelezo au connection kati ya graphs moja na nyingine. Pia unaweza tumia tables au charts kueleza mawazo yako hapa, ni wewe tuu na mapangilio wako, ukiona unafaa na kuleta maana.

Asante kutazama video hii, usiache kushare, kulike na kucomment na pia tembelea website ya Yesaya Software.

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

How to Create Logo in Illustrator and using Custom Brushes

How to Create Logo in Illustrator and using Custom Brushes

In this tutorial we are going the Logo in Adobe Illustrator and playing around the …