Home / Web Design / Namna Nitavyofanyia Kazi Mapendekezo ya Utafiti wa Namna Tunavyoshika Vifaa Vyetu vya Mawasiliano

Namna Nitavyofanyia Kazi Mapendekezo ya Utafiti wa Namna Tunavyoshika Vifaa Vyetu vya Mawasiliano

Ni matumaini yangu uko vyema kabisa. Tayari nimeanza fanyia kazi mapendekezo yaliotolewa kwenye article ya “How We Hold Our Gadgets” iliyo andikwa na Josh Clark – 2015.

Imeelezwa kwenye article hii kuwa bwana Steven Hoober mwaka 2013 alifanya utafiti kuangalia namna ambavyo tunashika vifaa vyetu vya mawasiliano. Aliweza kuchunguza watu wapatao 1,300 kuona ni namna gani wanashika vifaa hivi.

Hapa chini nimeweka picha ya matokeo aliopata na unaweza tumia muda wako kujichunguza na kuchunguza ndugu na marafiki kisha unaweza jiweka na kuweka wengine kwenye hayo makundi.

 

Katika kujibu article hii, utafiti umeonyesha maeneo ambayo ni rahisi yafikia tunaposhika vifaa vya mawasiliano.

Hapa chini nimeweka picha inayoonyesha maeneo yalio rahisi yafikia tunapotumia vifaa vya mawasiliano na amini na wewe unaweza tumia muda wako fanya utafiti kidogo maeneo unayo yafikia kwa urahisi unapotumia kifaa chako.

Sasa basi katika kufanyia kazi mapendekezo na matokeo ya utafiti huu kuna jambo moja nimejifunza. Kwenye website nyingi hasa “Responsive Website” menu button imekuwa ikiwekwa juu. Unaweza tembelea website ya Yesaya Software kuona namna ambayo menu button inatokea ukiwa kwenye kifaa kama simu au tablet.

Lakini kwenye article hii, imeonyesha kuwa eneo la juu ambapo imezoeleka wekwa menu button ni eneo gumu lifikia. Unaweza jaribu na ni kweli utaona inaleta shida kidogo fikia menu button na website nyingi tumezitengeneza hivyo kwa muda sasa.

Hapa chini niweka design ambayo ndio tutaifanyia kazi katika kutengeneza WordPress Theme from scratch. Kwenye design hii tutafanya marekebisho ya namna ya kuweka menu button kwenye namna ambayo itakuwa rahisi fikia.

Ungana nami kwenye videos nitazo zitoa hivi karibuni, tumia muda wako pitia website ya Yesaya Software kuna jambo jipya utajifunza.

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Beginners or those who have taken a break from web design for a few years …