Home / Web Design / 2. Kuinstall WordPress

2. Kuinstall WordPress

Tunaanze andaa mazingira ya kazi yetu, yaani kutengeneza WordPress Theme from Scratch. Hatua ya kwanza nitaingia kwenye website ya WordPress na kudownload WordPress.

WordPress ikimaliza download nita extract WordPress zip folder, na baada ya hapo nita cut kwa Ctrl + X, kisha nitapeleka folder hili kwenye folder la www ndani ya WAMP. Nitapaste folder la WordPress na kurename kuwa “upendo”, wewe unaweza rename kuwa vyovyote unavyotaka. Nina Imani tayari una WAMP tayari na umesha install.

Nitachek kama WAMP yangu inafanya kazi, ukiona iko kijani ujue inafanya kazi vuzuri. Sasa basi nitaenda tengeneza database, na hapa mimi ninatumia Navicat. Unaweza tumia phpMyAdmin inayokuja na WAMP. Database hii itatunza taarifa zote kwenye website yetu. Kwa sasa hakuna tables hapa WordPress itatengeneza wakati wa installation.

Hapa kwenye browser nimetumia virtual host kuweka hii “upendo.dev”, website yako unaweza ipata kupitia localhost/upendo. Kuna videos hapa Yesaya Software tayari nimeeleza namna ya kutengeneza virtual host.

Nikifungua website yangu napelekwa kuanza installation ya WordPress, form hii ya kwanza inahitaji taarifa kuhusu database nitajaza hizi taarifa kuhusu database name kuwa “upendo”, username “root”, password weka ulioweka default inakuwa blank, nitaacha host kuwa localhost na table prefix nitajaza “up”.

Hatua inayofuata nitajaza form ya taarifa za website nitajaza “Upendo” kama Site Title, username “Yesaya”, nitajaza password na kumalizia na email, kisha nita “Install WordPress”.

Ikimaliza nitapewa taarifa fupi, na nitabonyeza login nitaingiza username na password kisha nitalogin. Oooh vizuri sana, lakini hapa nimeona kuna update moja ya plugin, ni vizuri kuwa update hivyo nita update hii. Kama wewe hujaona hii update basi huna update na uko up-to-date.

Usiache kushare, kulike na kutoa maoni na kutembelea website ya Yesaya Software tukutane kipindi kijacho tuone namna ya kuinstall Starter Theme.

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Beginners or those who have taken a break from web design for a few years …