Home / Web Design / 3. Kuinstall Starter Theme & Taarifa za Majaribio

3. Kuinstall Starter Theme & Taarifa za Majaribio

Tumefanikiwa install WordPress, sasa twende Apperance kisha Themes. Hapa tunaona themes tatu zinazokuja na WordPress, Twenty Sixteen, Twenty Fifteen na Twenty Fourteen.

Nitatembelea website ya underscores.me, Underscores ni WordPress Theme Generator, ambayo inatupa WordPress Starter Theme. Ni theme ambayo haijawa styled kabisa ila ina mafile yote muhimu ya WordPress.

Nitajaza jina la Theme kuwa “Upendo”, kisha nitaclick hapa chini “Advanced Options”, nitajaza Theme Slig kuwa “upendo” ila sasa kwa herufi ndogo. Hapa kwenye Author URL, nitajaza link ya profile yangu ya LinkedIn. Na kisha nitaandika kidogo description kuhusu theme hii.

Hapa chini kuna option ya “sassify”, mimi nitachagua option hii sababu ndio modem way ya kuandika website style. Unaweza acha na ukaandika style kwa CSS, kisha nita Generate Theme.

Ikimaliza kudownload nitaextract folder hili kisha nitacut, nitaenda kwenye folder la wamp, kisha www, nitaingia kwenye folder la upendo, kisha wp-content, themes na nitapaste hapo.

Nitarudi kwenye browser, nitarefresh nitaona kuna theme imeongezeka hapa. Nitaangalia Theme details na nitapata taarifa kuhusu theme hii. Nita activate theme hii, na kisha nitatembelea website hii.

Unaweza ona vitu haviko styled, lakini ondoa shaka hili ndilo tunalotaka ili tuweze style theme vile sisi tunataka.

Nitarudi kwenye Administration Panel ili tuweza weka taarifa za majaribio. Nitaenda tools, kisha import, nitachagua WordPress na nita install plugin hii, ikimaliza nita activate & run importer.

Sasa WordPress wametengeneza data za majaribio, na wameweka taarifa ndani ya page ya Theme Unit Test ndiko utapata file la xml. Ambalo lina data za majaribio, nitalidownload na kufuatilia path yake wapi lipo.

Nitarudi kwenye browser, nitachagua file nililodownload, kisha nitali upload. Hapa nita assign hizi taarifa kwa user “Yesaya” na nitatick option ya “download and import file attachments”, kisha nita submit. Itachukua muda kidogo, ikimaliza utapata ujumbe, kisha bonyeza “Have fun” kurudi kwenye Dashboard.

Tutatembelea website sasa tuone, ukifika hapa utaona kuna post nyingi kweli, na hizi zimetengenezwa na WordPress wenyewe, kutizamia mambo mengi na aina mbalimbali za post na zitakavyoonekana. Hivyo ni kazi kwetu kuziweka katika muonekano mzuri.

Tukutane kipindi kijacho tukianza weka mazingira sawa kwa ajili ya kustyle theme yetu kwa sass.

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Beginners or those who have taken a break from web design for a few years …