Home / Web Design / 4. Kuinstall Grunt & SASS

4. Kuinstall Grunt & SASS

Ili kuweza kutumia SASS kupitia Grunt kwenye computer yenye Windows, ni lazima kwanza tuinstall SASS na Grunt. Hizi application zinahitaji mazingira maalum ili ziweze fanya kazi vizuri.

Sasa basi kuzifanya zifanye kazi, ni lazima tuweke dependencies zake. Grunt inakuwa installed kwenye computer kupitia Node Package Manager, au npm kwa kifupi. Kwenye Mac, Node na npm ziko installed tayari lakini kwenye computer yenye window ni lazima tuinstall wenyewe. Node Package Manager ni sehemu ya Node.js Javascript Platform. Sasa ili npm ifanye kazi na tuweze install Grunt ni lazima tuinstall NodeJS.

Hali kadhalika SASS ni Ruby Application, na inakuwa installed kwa kitu kinaitwa Ruby Gem. Hii inamaanisha, ili SASS ifanye kazi kwenye computer, ni lazima tuinstall Ruby kwanza.

Hii unaweza ona ni ngumu kidogo, na ni kweli kuna ugumu fulani. Lakini hii ni jambo la kufanya mara moja, kwa maana ukisha install Node na Ruby kwenye computer yako. Basi zitakuwa zinapatikana by default kwenye command line.

Node.js ninapatikana kwenye website ya nodejs.org, fungua website hii na udownload na kuinstall nodejs kwa hatua za kawaida kabisa. Ruby inapatikana kupitia website ya ruby-lang.org, lakini kupata installer ingia kwenye website ya rubyinstaller.org na kisha install kwa hatua za kawaida kabisa kuinstall.

Ngoja tumalizie hapa kwa kuinstall Grunt Command Line Interface (CLI), kwa kuingia kwenye command line na kuandika npm install -g grunt-cli. Hakikisha unapofungua command line, umerun kama Administrator. Baada ya hapo andika gem install sass ili kuinstall SASS

Usiende mbali bado tunaendelea kuweka mazingira vizuri ili tuweze kustyle theme yetu kwa SASS

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Take Your CSS Experience to the Next Level with SASS

Beginners or those who have taken a break from web design for a few years …