Home / Programming / Laravel / MVC Ndani ya Laravel

MVC Ndani ya Laravel

Kwenye video hii kuna jambo muhimu sana tumejadili, jambo hili ni MVC. Kama wewe ni Developer na bado hujasikia neno hili ninakuasa sasa fanya hima upate uelewa zaidi juu ya hili kwa kuanza na kutaza video hii. Kama umesikia na pengine umefanya kazi na MVC basi itakuwa vizuri ukitumia takribani dakika tatu jikumbusha mambo kadhaa kwenye MVC.

MVC ni kifupi cha maneno Model – View – Controller, hii tunaita ni Architectural/Design Pattern ambayo kwa kifupi inaugawa utengenezaji wa mfumo katika makundi matatu ambayo ndio Model, View na Controller.

Ukiangalia video hii tumeeleza kuwa Model inasimamia na kufuatilia taarifa za mfumo, wakati View inatoa matokeo na muonekano halisi wa mfumo kwa mtumiaji, na Controller ikiwa katikati ya Model na View kuhakikisha taarifa inayotoka kwenye Model au View ni lazima ipite kwenye Controller.

Karibu sana ufuatilie video hii na utapata kujua maswala mengine tuliogusia hapa na kuweka uhusiano kati ya Laravel na MVC.

About Yesaya R. Athuman

Colleagues know me as a highly Creative Software Developer who can always be trusted to come up with the new approach. But I know that client's business come first, and I never try to impose my ideas on others. Instead, I spend a lot of time understanding business and the audience before suggesting ideas. I can (and often do) work well alone, but I'm at my best collaborating with others.

Check Also

The Use of Artificial Intelligence in solving challenges of Sexual Reproductive Health in Tanzania

Many years ago, in our Tanzanian culture, youths used to talk with their aunts sensitive/very …